SOKA

Chelsea yajipanga kwa mashambulizi dhidi ya Manchester United

Reuters

Mlinda mlango wa klabu ya soka ya Chelsea, David Luiz amewaonya Manchester United kuwa timu yake imepania kuwapa maumivu zaidi wakati watakapokutana katika mechi yao inayopigwa hii leo jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Vigogo hao wa soka wanatarajia kuumana katika mechi ya robo fainali ya kombe la shirikisho FA huku kila mmoja akijigamba kuibuka kinara wa mchuano huo.

Mambo bado hayajakaa sawa upande wa Chelsea ambao wananolewa na Rafael Benitez baada ya kupata kichapo cha bao 1-0 siku ya alhamisi katika ligi ya Ulaya.

United wanashuka dimbani hii leo wakiwa na Wayne Rooney ambaye hakushiriki mtanange uliopita wa siku ya jumanne katika mechi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid.