SOKA

Issa Hayatou kuwania tena Urais wa CAF

Shirikisho la soka barani Afrika CAF kwa mara nyingine tena limemteua Rais wake wa sasa Issa Hayatou kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa shirikisho hilo na anatarajiwa kuongoza kwa miaka mingine minne zaidi.

AFP PHOTO / FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Baada ya uteuzi wake Hayatou amesema ameisifu nchi ya Morocco kuwa imekuwa kiungo muhimu katika soka la Afrika na amesema anafarijika kuwa hapo kwani kwa mara ya kwanza aliteuliwa kushika wadhifa huo mwaka 1988 akiwa katika nchi hiyo.

Wageni waliohudhuria mkutano wa CAF uliofanyika siku ya jumapili nchini Morocco ni pamoja na Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter ambaye alimpa cheti cha heshima Issa Hayatou.

Hayatou ambaye ni raia wa Morocco ana umri wa miaka 66 na ameongoza shirikisho hilo kwa miaka 25 na anatarajia kustaafu wadhifa wake itakapofika mwaka 2017.