SOKA

Manila Fernando apigwa marufuku kujihusisha na soka kwa siku tisini

Shirikisho la soka duniani FIFA limempiga marufuku Manilal Fernando ambaye ni mmoja wa wanachama wa Kamati Kuu ya Shirikisho hilo kutoshiriki katIka shughuli zozote za soka kwa muda wa siku 90.

Matangazo ya kibiashara

Fernando raia wa Sri Lanka anatuhumiwa kukiuka maadili ya FIFA baada ya kujihusisha na rushwa kwa kujaribu kununua kura za urais katika uchaguzi wa shirikisho hilo mwaka 2011.

Fernando mwenye umri wa miaka 63 amekuwa ni mwakilishi wa shirikisho la soka barani Asia AFC katika kamati hiyo kuanzia mwaka 2011.

Uchunguzi dhidi yake umekuwa ukifanywa tangu mwaka 2012 na kusimamishwa kwake.