Barcelona yatinga robo fainali ligi ya mabingwa baada ya kuichakaza AC Milan
Klabu ya Barcelona ya Uhispania imedhirisha msemo wa waswahili kuwa kutangulia sio kufika baada ya kufuzu katika robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa kwa kuigaragaza AC Milan ya Italia mabao 4 kwa 0 jana usiku.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Mashabiki wa Barcelona watamkumbuka sana Lionel Messi ambaye aliifungia Barcelina mabao mawili katika mchuano huo.
Wengi walikuwa wametabiri kuwa huenda Barcelona wangetolewa nje ya michuano hiyo baada ya kufungwa na AC Milan mabao 2-0 katika mchuano wa kwanza waliocheza ugenini mwezi uliopita.
Mabao mengine ya Barcelona yalipachikwa na David Villa aliyefunga la tatu katika dakika ya 55 huku Jordi Alba akifunga bao la mwisho katika dakika za lala salama la mchuano huo.