SOKA-ULAYA

Arsenal yatupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya

Hatimaye klabu ya soka ya Uingereza ya Arsenal imebanduliwa nje ya michuano ya soka ya klabu bingwa barani Ulaya licha ya kupambana na kupata ushindi wa mabao 2-0 ya ugenini dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani.

Matangazo ya kibiashara

Mabao ya Arsenal yalitiwa kimyani na Olivier Giroud na Laurent Koscielny.

Huu ni msimu wa nane mfululizo kwa Arsenal the Gunners kushindwa kufika katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema amesikitishwa kwa vijana wake kuondolewa katika mashindano hayo lakini amewapongeza kwa kujituma na kunyakua ushindi huo wa ugegeni.

Buyern Munich wamefanikiwa kutinga katika hatua hiyo baada ya ushindi wao wa mabao 3-1 wa ugenini huko Uingereza.