MISRI

Mashabiki wa soka waandamana nchini Misri

Mamia ya mashabiki wa soka nchini Misri wameandamana nje ya ofisi ya mwendesha mashitaka ya umma hii leo, wakidai kuachiwa huru kwa mashabiki wenzao wa kundi la Ultras.

Mashabiki wa soka wakiandamana
Mashabiki wa soka wakiandamana telegraph.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa kundi hilo wakiimba na kupiga makofi kwa pamoja wamefunga eneo zima linalozunguka ofisi ya mwendesha mashtaka katikati mwa jiji la Cairo wakisisisitiza kuachiwa kwa wenzao 38 waliokamatwa katika jimbo la Nile Delta la Menufia baada ya kubainika kuwa wafuasi wa kundi la uhalifu.

Juma hili mwendesha mashtaka pia aliwakuta na kosa la kujaribu kuchoma moto mahakama na kuwanyanyasa wafanyakazi wake, wakati mmoja wa wafafuasi wao Gamal Helal akihojiwa ndani.

Kukamatwa kwa wafuasi wa Ultras ilikuwa ishara ya kwanza ya ukandamizaji kwenye taasisi yenye nguvu ambayo ilikuwa nguvu kubwa ya kisiasa wakati wa maandamano ya nguvu ambayo yalimwangusha Hosni Mubarak mwaka 2011.