TENNIS

Rafael Nadal anyakua taji la India Wells

Rafael Nadal ndiye bingwa wa India Wells katika mchezo wa Tennis baada ya kumshinda Juan Martin del Potro raia wa Argetina kwa seti za 4-6 6-3 6-4.

Matangazo ya kibiashara

Nadal ameshinda taji hilo baada ya jeraha la goti na ushindi wake nchini India unamwongezea mataji aliyopata kuanzia mwezi wa Februari mwaka huu nchini Brazil na Mexico.

Hata hviyo, Nadal hatashiriki katika michuano ya Miami nchini Marekani itakayofanyika wiki ijayo kutokana na kalenda aliyonayo katika michuano itakayofanyika barani Ulaya.

Raia huyo wa Hispania amewashukuru mashabiki wake kwa kumuunga mkono huko India akisema kuwa lilikuwa wiki gumu sana kwake katika mashindano hayo licha ya kunyakua ushindi huo.

Nadal ambaye amenyakua mataji makuu 11 alishinda taji kuu mara ya mwisho mwaka 2010.

Rafael Nadal ni wa nne duniani katka orodha ya wachezaji wa mchezo huo duniani kwa upande wa wanaume.