Soka

Rio Ferdinand ajiondoa katika kikosi cha timu ya taifa ya soka ya Uingereza

Mchezaji wa safu ya nyuma ya klabu ya Mancester United ya Uingereza Rio Ferdinand amejiondoa katika kikosi cha Uingereza kinachojiandaa kwa michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya San Marino na Montenegro.

Matangazo ya kibiashara

Kocha wa Uingereza Roy Hodgson alikuwa amemwita Ferdinand kwa mara ya kwanza katika kikosi cha Uingereza lakini licha ya kujiondoa katika kikosi hicho amemwambia Kocha Hodgson kuwa ataendelea kucheza  michuano ya Kimataifa.

Aidha, kocha huyo amesema kuwa amesikitishwa mno na uamuzi huo wa Ferdinand ambaye alikuwa anategemewa katika kikosi hicho .

Fedirnand mwenye umri wa miaka 34 aliichezea Uingereza kwa mara ya mwisho katika michuano ya kufuzu kwa kombe la Ulaya nchini Uswizi mwaka 2011.

Nafasi ya Ferdinand ambaye amechezea Ungereza mara 81 sasa itachukuliwa na Steven Caulker anayechezea klabu ya Tottenham Hotspur .

Wachezaji wengine waliondolewa katika kikosi cha Uingereza kwa sababu ya majeraha ni pamoja na Michael Dawson na Aaron Lennon wanaochezea klabu ya Tottenham Hotspurs.

Uingereza itachuana na San Marino siku ya Ijumaa kabla ya kumenyana na Montenegro Jumanne juma lijalo.

Kikosi cha Uingereza kinawajumuisha Makipa: Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City), Fraser Forster (Celtic/SCO)

Walinzi : Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Steven Caulker (Tottenham Hotspur), Ashley Cole (Chelsea), Glen Johnson (Liverpool), Joleon Lescott (Manchester City), Chris Smalling (Manchester United), Kyle Walker (Tottenham Hotspur)

Viungo wa Kati : Michael Carrick, Tom Cleverley (both Manchester United), Steven Gerrard (Liverpool), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Manchester City), Leon Osman (Everton), Scott Parker (Tottenham Hotspur), Alex Oxlade-Chamberlain, Theo Walcott (both Arsenal), Ashley Young (Manchester United)

Washambulizi: Jermain Defoe (Tottenham Hotspur), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United)