SOKA

DR Congo kujaribu kusitisha rekodi ya Libya ya kutofungwa katika michuano ya soka ya kufuzu kwa kombe la dunia

Timu ya taifa ya soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itachuana na Libya Jumapili hii katika uwanja wa Kimataifa wa Stade de Martyrs jijini Kinshasa katika mchuano wa kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Libya itakuwa ugenini kutetea rekodi yake ya kutoshindwa katika michuano hiyo ambapo hadi sasa inaongoza kundi lao kwa alama nne baada ya ushindi na sare katika mechi zake mbili zilizopita.

Libya walianza kampeni zao kwa mguu wa kulia baada ya kuifunga Cameroon mabao 2 kwa 1 nyumbani na baadaye kulazimisha sare ya bao 1 kwa 1 na Togo mjini Lome.

Shirikisho la soka nchini Libya limeanza mazungumzo na kocha wa zamani wa Misri Hassan Shehata kumwajiri kama mkufunzi wa timu hiyo inayosaka nafasi ya kufuzu kwa kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia ya kandanda nchini humo.

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo nayo  ni ya pili katika kundi hilo na alama 3 baada ya kushinda mchuano wake wa kwanza na ikiwa itashinda mchuano wake dhidi ya Libya itaongoza kundi hilo ikiwa Togo itaishinda Cameroon.

DR Congo alimaarufu kama Leopard ambayo inaorodheswa ya 79 duniani ilifuzu kombe la dunia mara moja tu mwaka 1974.