MICHEZO

Harambee stars yaitunishia kifua Super Eagles

vijana wa Kenya Hambee Stars wakimenyana na Super Eagles ya Nigeria
vijana wa Kenya Hambee Stars wakimenyana na Super Eagles ya Nigeria goal.com

Timu ya soka ya taifa la Kenya Harambee stars jana Jumamosi imeonesha mchezo mzuri katika mtanange dhidi yake na Super Eagles ya Nigeria licha ya mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 

Matangazo ya kibiashara

Harambee Stars licha ya kupata mateso tangu wawasili nchini Nigeria kucheza na Super eagles katika mechi ya kufuzu kushiriki michuano ya kombe la dunia, iliongoza kwa kupata goli moja hadi dakika za majeruhi ambapo mchezaji Nnamdi Oduamadi alipoiondolea Super Eagles aibu kwa kufunga bao na punde tu Kipyenga cha mwisho kumaliza mechi kikapulizwa.

Katika mtanange huo uliopigwa mjini Calabar Nigeria, Harambee Stars ilikuwa ya kwanza kuona nyavu za Super Eagles kupitia kwa mchezaji wake Francis Kahata katika dakika ya 36 kipindi cha kwanza.

Hii leo michuano ya kusaka nafasi ya kufuzu kushiriki kombe la dunia mwaka ujao huko nchini Brazil inaendelea ambapo timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars inashuka dimbani kumenyana na timu ya taifa ya Morocco katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.