GOFU-PGA TOUR

Tiger Woods arejea kwenye nafasi ya kwanza kwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa Gofu duniani

Mchezaji Tiger Woods amefanikiwa kurejea kwenye kilele cha uchezaji bora wa mchezo wa Golf duniani baada ya kufanikiwa kutwaa taji la Arnold Palmer. 

Mchezaji nambari moja wa mchezo wa Golf duniani, Tiger Woods akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi
Mchezaji nambari moja wa mchezo wa Golf duniani, Tiger Woods akifurahia mara baada ya kutangazwa mshindi Reuters
Matangazo ya kibiashara

Woods amefanikiwa kurejea kwenye nafasi ya kwanza kwa ubora wa mchezo huo na kufanikiwa kumpiku Rory Mcllroy aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo kwa muda sasa toka mchezaji huyo awe nje.

Haya ni mashindano yake ya 77 kwa Tiger Woods kushiriki ambapo ni taji lake la tatu kushinda katika mashindano yaliyofanyika mwaka huu.

Mashindano mengine ambayo Tiger Woods amefanikiw akushinda kwa mwaka huu ni pamoja na lile la Doral na Torrey Pines na sasa analenga kufanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya Masters yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi wa nne mwaka huu.

Mara baada ya kushinda taji hilo, Woods amesema hakutarajia ushindi huo licha ya kucheza kwa kujiamini na kwamba alitumia makosa ya wapinzani wake kufanya vizuri zaidi.

Toka mwaka 2010 mwezi October Tiger Woods alikuwa nje ya mchezo huu kutokana na kashfa ya kuwa na uhusiano nje ya ndoa yake uliomfanya asimame kwa muda kujenga upya familia yake na jina lake.

t was Woods's sixth title in his last 20 starts on the PGA Tour, and after wins at Doral and Torrey Pines this year, he is now clear favourite to capture his fifth Masters title when the season's opening major begins at Augusta on 11 April.