WORLD CUP QUALIFICATIONS-UEFA

Uingereza kuwakabili Montenegro, Ufaransa kibaruani na Uhispania katika mechi za kufuzu kucheza kombe la dunia mwakani nchini Brazil

Mechi za kuwania kufuzu kukata tiketi ya kucheza fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014 barani ulaya zinatarajiwa kuchezwa hii leo kwa miamba mbalimbali kushuka viwanjani kupepetana.

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wakiingia kwenye uwanja wa mazoezi tayari kwa mchezo wao wa leo usiku
Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wakiingia kwenye uwanja wa mazoezi tayari kwa mchezo wao wa leo usiku Reuters
Matangazo ya kibiashara

Mechi ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa ni ile ambayo itazikutanisha timu za taifa za Uingereza ambao watakuwa na kibarua dhidi ya timu ya taifa ya Montenegro ambapo katika mchezo wa awali timu hizo zilitoka suluhu huku mshambuliaji Wyne Rooney akipewa kadi nyekundu.

Mchezo huo ni wa kundi H ambapo katika mechi nyingine Ukraine watacheza na Moldova wakati Poland watakuwa na kibarua dhidi ya San Marino.

Katika kundi B, Armenia watacheza na Jamhuri ya Czech, wakati Denmark wao watakuwa nyumbani kuwakabili Bulgaria huku mchezo mwingine ni ule kati ya Malta na Italia.

Mchezo mwingine ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka barani Ulaya ni ule ambao utaikutanisha timu ya taifa ya Ufaransa watakaokuwa nyumbani kuwakaribisha Uhispania kwenye mchezo ambao unatarajiwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili.