LIGI KUU YA TANZANIA

Azam yazidi kuinyemelea Yanga, Simba yaangukia pua mjini Bukoba, Kagera

Ligi kuu ya Vodacom nchini Tanzania, imeendelea kushika kasi wakati huu ikielekea ukingoni huku vinara wa ligi hiyo Yanga wakiendelea kufukuzwa kwa ukaribu na Azam FC, huku mabingwa watetezi Simba wakiendelea kujikongoja.

Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche
Mshambuliaji wa Azam FC, Kipre Tchetche RFI
Matangazo ya kibiashara

Kayika mechi ambazo zilichezwa siku ya Jumatano kwenye viwanja viwili tofauti, timu ya Azam ambayo inawania kutwaa taji la msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom nchini Tanzania, ilikuwa na kibarua dhidi ya Prisons ya Mbeya.

Kwenye mchezo huo Azam walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Prisons mchezo ambao umeshuhudia mchezaji Kipre Tchetche, Salum Abubakar na John Bocco wakiipa ushindi timu yao.

Mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Azama wa Chamazi ulioko nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Kwingine timu ya Kagera Sugar iliwakaribisha mabingwa watetezi wa kombe hilo Simba kwenye mchezo ambao umeshuhudia mabingwa hao watetezi wakiangukia pua kwa kukubali kipigo cha bao 1-0.

Kwa matokeo hayo simba inaendelea kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi kwa kuwa na alama 34, huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Azam yenye alama 40 huku Yanga ambao ni vinara wa ligi hiyo wakia na alama 48.

Timu zinazoshikilia mkia na ambazo ziko kwenye hatari ya kushuka daraja ni pamoja na Polisi Morogoro, Toto African na Mwanza na Africa Lyon.

Azam and Simba remain second and third with 40 and 34 points respectively while Kagera sugar Move upto fourth with 34 point.