RIADHA-PISTORIUS

Oscar Pistorius huenda akashiriki mashindano ya dunia ya mwezi wa 8 baada ya kuruhusiwa kusafiri nje ya nchi yake

Mwanariadha wa Afrika Kusini mwenye ulemavu, Oscar Pistorius
Mwanariadha wa Afrika Kusini mwenye ulemavu, Oscar Pistorius REUTERS/Siphiwe Sibeko

Mwanariadha mwenye ulemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius ambaye yuko nje kwa dhamana huenda akashiriki mashindano ya dunia ya riadha yatakayofanyika mwezi wa nane baada ya kuruhusiwa na mahakama kusafiri.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja kufuatia mawakili wa Pistorius kuwasilisha pingamizi kwenye mahakama ya mjini Pretoria wakipinga dhamana ya awali iliyotolewa kwa mwanariadha huyo ambayo ilimkataza kutosafiri nje ya nchi hiyo.

Katika uamuzi wake mahakama iliyokuwa inasikiliza pingamizi la Pistorius imesema uwa imeridhika na utetezi wa mawakili wa utetezi na kwamba haioni hatari ya mwanariadha huyo kusafiri nje ya nchi yake.

Pistorius mwenye umri wa maiaka 26 ameshtakiwa kwenye mahakama ya mjini Pretoria kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake, Reeva Steenkamp wakati wa siku ya wapendanao kwa kumpiga risasi zilizomtoa uhai.

Awali mahakama hiyo ilimtaka mwanariadha Pistorius kuwasilisha hati yake ya kusafiria.