Michezo-Football

Manchester United yazidi kupiga hatua

Klabu ya Manchester United imeendelea kuchupa hatua kwa hatua kuelekea kunyakua taji lake la ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya 20 baada ya kupata ushindi mwepesi wa bao 1-0 dhidi ya Sunderland. 

Matangazo ya kibiashara

Bao hilo la lilipatikana katika kipindi cha kwanza kupitia mkwaju wa Van Persie uliokua ukielekea nje na kumgonga beki wa Sunderland Titus Bramble na kuishia kimyani na hivyo kuifanya Man.United kusalia kileleni ikiwa na pointi 77.

Man United inafuatiwa na klabu ya Manchester City ikiwa nyuma kwa pointi 15 kufuatia ushindi wake wa bao 4 -0 dhidi ya Newcastle United kwenye uwanja wa Etihad.