UINGEREZA

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers anajiandaa kuanzisha mazungumzo na Steven Gerrard juu ya kumuongezea mkataba

Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard akishangilia goli alilofunga dhidi ya Aston Villa
Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard akishangilia goli alilofunga dhidi ya Aston Villa

Kocha Mkuu wa Liverpool Brendan Rodgers amesema yupo tayari kuanzisha mazungumzo na Nahodha wake Steven Gerrard kujadili mpango wa kumuongezea mkataba aendele kusalia kuitumia Klabu hiyo. Rodgers amesema agenda kuu kwake kwa sasa ni kuhakikisha anamshahiwi Kkungo huyo wa Kimataifa wa Uingereza Gerrard anaongeza mkataba na kuwatumikia Vijogoo vya Jiji kwa muda mwingine.

Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo wa Liverpool amesema hana hofu ya aina yoyote ya kwamba Gerrard anaweza akaendelea kucheza akiwa na miaka zaidi ya thelathini kutokana na kiwango ambacho amekuwa akikionesha hivi karibuni.

Kauli ya Rodgers imekuja baada ya Gerrard kuisaidi Liverpool kufanikiwa kushinda katika mchezo wao wa jumapili dhidi ya Aston Villa ambapo alifunga goli la pili kwa mkwaju wa penalty na kuokoa mpira mmoja uliokuwa unaingia kwenye golini mwao.

Gerrard mwenye umri wa miaka 32 akiwa amecheza michezo 625 na alikuwa mchango mkubwa kwa Liverpool kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa ambapo waliibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Rodgers amekiri Gerrard ni mtu muhimu sana kwenye kikosi chake hivyo hayupo tayari kumpoteza kiungo mahiri kama yeye na ndiyo maana wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha wanamuongezea mkataba.

Kocha Rodgers amesema licha ya Gerrard kuendelea kukabiliwa na majeruhi katika msimu huu lakini bado amekuwa mchango wa hali ya juu kwa Liverpool na kwa sasa wanaendelea kupigania nafasi ya kuwa kwenye sita bora.