MIAMI MASTERS-MAREKANI-UINGEREZA

Murray atwaa Taji la Miami Masters na kufanikiwa kushika nafasi ya Pili kwa Ubora wa Tennis Duniani upande wa Wanaume

Mchezaji nambari mbili kwa ubora wa Tennis upande wa wanaume Andy Murray amefanikiwa kushinda Taji la Miami Masters baada ya kumfunga David Ferrer kwenye mchezo wa Fainali.

Mchezaji Tennis Andy Murray akiwa ameshikilia Taji la Miami Masters baada ya kumfunga David Ferrer
Mchezaji Tennis Andy Murray akiwa ameshikilia Taji la Miami Masters baada ya kumfunga David Ferrer
Matangazo ya kibiashara

Murray amefanikiwa kuibuka na ushindi huo baada ya kushinda kwa seti mbili kwa moja za 2-6 akianza kufungwa kisha akaamka kutoka usingizini na kushindwa seti mbili kwa 6-4 na 7-6.

Murray mwenye umri wa miaka 25 hili linakuwa taji lake tisa huku mwenyewe akisema hayo yalikuwa maandalizi mazuri kwa ajili ya Masindano ya French Open akiwa na matumaini atafanya vizuri zaidi.

Mchezaji huo kutoka Uongereza alionekana amejiandaa vizru na kucheza mchezo wa kuvutia baada ya kupoteza seti ya kwanza na hivyo kumpa wakati mgumu mpinzani wake Ferrer.

Murray baada ya kupata ushindi huo amechumpa kutoka nafasi ya tatu hadi nafasi ya pili kwa ubora wa Tennis upande wa wanaume kitu ambacho kimemsukuma kusema anataka kufika nafasi ya kwanza.

Hii ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka karibu kumi kushuhudia nafasi mbili za juu hawapo manguli wa mchezo wa Tennis duniani ambao ni Roger Federer na mwenzake Rafael Nadal.

Kwa mujibu wa viwango vipya vya ubora vinaonesha nafasi ya kwanza imeshikiliwa na Novak Djokovic nafasi ya pili akiwepo mshindi wa Miami Masters Andy Murray huku nafasi ya tatu ikienda kwake Roger Federer.

Nafasi ya nne imeangukia mikononi mwa David Ferrer aliyefungwa kwenye fainali ya Miami Masters huku Rafael Nadal yeye akiwa kwenye nafasi ya tano huko nafasi ya sita ikishikiliwa na Tomas Berdych.

Raia wa Argentina Juan Martin Del Porto yeye amekamata nafasi ya saba akifuatiwa na Jo-Wilfried Tsonga huku Mfaransa Richard Gasquet akinyakua nafasi ya tisa na kumi boa inafungwa naye Janko Tipsarevic.