Kocha wa Tottenham Villas-Boas anahisi maumivu aliyoyapata Kiungo wake Bale hayatokuwa makubwa

Kiungo wa Tottenham Gareth Bale akiugulia maumivu baada ya kuumia kiwiko cha mguu kwenye mchezo dhidi ya Basel
Kiungo wa Tottenham Gareth Bale akiugulia maumivu baada ya kuumia kiwiko cha mguu kwenye mchezo dhidi ya Basel

Klabu ya Tottenham imeanza kuingiwa na hofu ya kumkosa kwa muda mrefu Kungo wake wa Kimataifa wa Wales Gareth Bale aliyeumia kiwiko cha mguu kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Michuano ya Europa. Kocha Mkuu wa Tottenham Andre Villas-Boas amesema anasubiri kauli ya madakatari wanaomfanyia uchunguzi lakini anaimani maumivu aliyoyapata Bale hayatakuwa makubwa sana.

Matangazo ya kibiashara

Villas-Boas amekiri kukumbwa na hofu kutokana na Kiungo wake bale kuumia kwenye mchezo wa Robo Fainali ya Michuano ya Europa dhisi ya Basel uliomaliza kwa sare ya magoli 2-2.

Kocha huyo amesema Madakatari ndiyo watawaondoa hofu kwa kueleza maumivu aliyoyapata Bale ni ya kiasi gani na atakuwa nje ya uwanja wa kipindi gani kabla ya kurejea dimbani.

Villas-Boas amekiri kupitia Televisheni tukio hilo lilikuwa baya sana lakini anaamini maumivu aliyoyapata Bale hayatokuwa mabaya kama ambavyo yeye aliliona tukio hilo kwenye picha.

Bale alilazimika kuondolewa uwanjani kwa kutumia kitanda cha wagonjwa baada ya kushindwa kusimama kufuatia maumivu makali aliyoyapata baada ya kuumia kiwiko cha mguu.

Kiungo huyo ambaye yupo kwenye kiwango kizuri msimu huu ameshafunga jumla ya magoli 27 kwenye mchezo 45 aliyocheza akiwa na Timu yake ya Taifa ya Wales pamoja na Klabu yake ya Tottenham.

Villas-Boas amewaondoa hofu mashabiki na kuwataka kuwa watulivu kusubiri taarifa ya Madaktari wa Timu hiyo ambao wanamfanyia uchunguzi na taarifa yao itatolewa jioni ya Ijumaa.