SOKA

Arsenal kushuka dimbani kukabiliana na West Brom jumamosi hii

RFI

Kocha wa klabu ya soka ya Arsenal, Arsene Wenger amesema bado hajakata tamaa hata kama kikosi chache hakijashika nafasi miongoni mwa timu nne zinazoshika nafasi ya juu katika ligi ya mabingwa msimu huu.

Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Wenger inakuja wakati huu ambapo Arsenal maarufu kama The Gunners ikitarajiwa kushuka dimbani leo jumamosi kukabiliana West Brom ambao watakuwa katika uwanja wa nyumbani.

Arsenal au wameshinda mechi tano kati ya sita za mwisho wa ligi kuu na kuvuna pointi 24 dhidi ya Manchester City ambao ndio wanaoongoza ligi hiyo.

Michezo mingine inayotarajiwa kupigwa hii leo ni kati ya Reading na Southampon, Norwich na Swansea wakati Aston Villa watakuwa na kibarua cha ugenini dhidi ya Stoke City.