Football

Timu ya taifa ya Ufaransa kukutana katika mechi ya kirafiki na Ubelgiji

vijana wa timu ya taifa ya Ufaransa ya mpira wa miguu
vijana wa timu ya taifa ya Ufaransa ya mpira wa miguu

Timu ya taifa ya Ufaransa les Blues watakutana katika mechi ya kirafiki na ubelgiji ifikapo Agosti 14 jijini Brussels, duru kutoka shirika la mpira wa miguu nchini Ufaransa FFF zimethibitisha

Matangazo ya kibiashara

kabla ya mechi hiyo, vijana wa Didier Deschamps watakuwa katika mzunguuko Amerika Kusini mwezi Juni kukiwa na mpango wa kucheza mechi mbili za kirafiki, tarehe 5 na Uruguay mjini Montevideo, na tarehe 9 Juni jijini Alegro na Brazil

baada ya hapo les blues wataendelea na mechi za mchuano wa kufuzu kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil kwa kumenyana na Georgia tarehe 6 septemba kabla ya kupepetana na Belarusi tarehe 10 mwezi Septemba.

Ufaransa na Ubelgiji zimekutana mara 51, mara ya mwisho ilikuwa Novemba 15 mwaka 2011 kwenye uwanja wa Stade de France katika mechi ya kitafiki ambapo timu hizo zilitoka sare ya kutofungana ya sufuri kwa sufuri.

Ubelgiji kwa sasa inawachezaji wazoefu kama vile Hasard, Witsel, Fellaini, Defour, Kompany na wengine.