FOOTBALL

chama cha soka nchini Uingereza cha ridhia matumizi ya teknologia ya kisasa viwanjani

Chama cha soka nchini Uingereza FA, kimeridhia mfumo wa matumizi ya teknologia ya kisasa ya kuchunguza bao kwa kutumia mitambo maalum katika msimu wa ligi kuu nchini humo wa mwaka 2013-2014.

Matangazo ya kibiashara

Kampuni ya Hawk-eye ya nchini uingereza ndui iliopewa jukumu la kutowa vifaa viavyo tumiwa baada ya mkutano wa viongozi wa vilabu ishirini hivi.

Peter Coates mwenyekiti wa klabu ya Stock City amesema ameridhia mfumo huo na wajumbe wengine wote wamekubali.

Kampuni ya Hawk-eye itaweka kamera katika viwanja vyote vinavyo tumiwa katika michuano ya ligi ili kuondowa ubishi ambao umekuwa ukiibuka mara kwa mara kuhusu bao kuingia au la.

Shirikisho la soka duniani FIFA upande wake kilichagua kampuni ya Ujerumani ya Goal Control ambayo itatumia mfumo huo wa kamera katika viwanja vya kombe la shirikisho nchini Brazil.

Mfumo huo umeanzishwa ili kumaliza ubishi, ambapo uchunguzi ulioendeshwa katika kaombe la dunia la mwaka 2010 nchini Afrika kusini ulionyesha kwamba bao la Franck Lampard mchezaji wa Uingereza dhidi ya Ujerumani lilikataliwa wakati lilikuwa tayari limevuka mstari wa bao