RAGA

Australia yajipanga kuchukua ubingwa wa raga michuano ya olimpiki 2016

dailytelegraph.com.au

Kamati ya mchezo wa raga nchini Australia AOC imedhamiria kuibuka miongoni mwa vinara watano wa kwanza wa mashindano ya olympic ya mwaka 2016 ambayo yatafanyika jijini Rio de Janeiro.

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti ya mwaka iliyotolewa ijumaa hii, Rais wa AOC John Coates amesema lengo lao ni kuhakikisha wanakuwa kati ya mataifa matano bora katika michuano hiyo ili waweze kunyakua medali nyingi zaidi.

AOC imetenga bajeti ya jumla ya dola za marekani milioni 31.4 sawa na dola za Australia milioni 29.8 kufadhili programu za michezo ya Rio ya mwaka 2016.

Australia ilijinyakulia medali 7 za dhahabu, 16 za fedha na 12 za shaba katika michuano ya olympic ya mwaka jana iliyofanyika jijini London, Uingereza.