SOKA

Arsenal yanuia kumaliza miongoni mwa timu nne bora katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza

Kocha wa Klabu ya Arsenal nchini Uingereza Arsene Wenger amewaambia wachezaji wake kuendelea kutia bidii ili kumaliza msimu huu wa soka kati ya nne bora. 

Matangazo ya kibiashara

Wenger ameongeza kuwa ushindi wa mwishoni mwa Juma lililopita wa mabao 3 kwa 1 dhidi ya Norwich umewapa matumaini ya kumaliza msimu huu katika nafasi nzuri ili kushiriki katika michuano ya kusaka ubingwa wa klabu bora barani Ulaya UEFA msimu ujao.

Arsenal ambayo ilikuwa katika nafasi ya tano kabla ya mchuano wa mwisho wa juma, sasa ni ya tatu kwa alama 59 alama moja zaidi dhidi ya Chelsea.

Arsenal watakuwa wenyeji wa Everton siku ya Jumatano katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates kuendelea kupambana kupata ushindi kujinyakulia alama zaidi kuwawezeha kusalia katika timu nne bora.

Timu zingine zinazopambana kumaliza katika nafasi nne bora ni pamoja na Chelsea na Tottenham ambazo zina alama 58 kila mmoja.

Manchester United iliyopata ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Stoke City mwishoni mwa juma, inaendelea kuongoza msururu wa ligi hiyo kwa alama 80 mbele ya Manchester City ambayo ni mabingwa watetezi ambao wana alama 65.

Kuhusu mchuano wa nusu fainali wa taji la shirikisho la soka nchini humo FA , Manchester City waliwafunga Chelsea mabao 2 kwa 1 Jumapili iliyopita.

Beki za Chelsea David Luiz amesema mshambulizi wa Manchester City Sergio Aquero anastahili kukiri kumchezea visivyo wakati wa mchuano huo na kufunga bao lililowapa ushindi City.

Manchester city sasa watamenyana na Wigan Athletic katika fainali ya taji hilo tarehe 11 mwezi wa tano katika uwanja wa Webley.