Soka

Mashabiki wa soka nchini Brazil wakabiliana kwa risasi

Mashabiki wawili wa mchezo wa soka waliuawa baada ya kupigwa risasi wakati wa mchuano wa ligi kuu ya soka nchini Brazil kati ya klabu ya Ceara na Forteleza.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wanasema kuwa mashabiki waliuawa walikuwa wa klabu ya Ceara waliokuwa wageni katika mchuano huo na walipigwa risasi na watu waliokuwa ndani ya gari lililokuwa limewabeba mashabiki wa Forteleza.

Aidha, imebainika kuwa mashabiki wa vlabu viwili walianza kukabiliana baada ya mashabiki wa klabu ya Ceara kuwashambua wenzao wa Fortaleza kwa mawe kabla ya kuzuka kwa ufwatuliaji huo wa risasi.

Watuhumiwa wa shambulizi hilo tayari wamekamatwa na polisi kwa uchunguzi zaidi.

Mchuano huo ulikamilika kwa majonzi baada ya wenyeji Forteleza kufungwa na Ceara bao 1 kwa 0 na kuzidisha uhasama wakati wa pambano hilo la soka.

Uwanja wa Arena Castelao kulikotokea shambulizi hilo utatumiwa wakati wa michuano ya kombe la dunia na ile ya Mashirikisho linaloaza mwezi Juni mwaka huu.