Soka

Manchester City na Wigan kumenyana kabla ya fainali ya kombe la FA

Manchester City na Wigan FC watamenyana katika mchuano wa ligi kuu nchini Uingereza kabla ya kuchuana katika fainali ya kombe la FA mwezi ujao katika uwanja wa Wembley.

Matangazo ya kibiashara

Wachambuzi wa soka wanaona kuwa mchuano huu wa Jumatano utakuwa kama wa majaribio wa fainali hiyo ya FA baada ya kufuzu fainali mwishoni mwa wiki iliyopita.

Manchester City wanajaribu kuwafikia viongozi wa ligi kuu nchini humo Manchester United ambao wana alama 15 zaidi dhidi yao katika msururu huo wa ligi.

Kocha wa Manchester City Roberto Mancini amesema ameridhika na uamuzi wa chama cha soka nchini humo kutomchukulia hatua mshambulizi wake Sergio Aguero ambaye alituhumiwa na David Luiz kwa kumchezea vibaya.

Wigan ambao wamefika katika fainali ya FA kwa mara ya kwanza katika historia yake ya soka wanapambana pia kusalia katika ligi kuu msimu ujao na wanasalia na kibarua dhidi ya Sunderland, Stoke na Aston Villa kujaribu kujikusanyia alama muhimu.

Arsenal nayo watakuwa wenyeji wa Everton siku ya katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates kuendelea kupambana kupata ushindi kujinyakulia alama zaidi kuwawezeha kusalia katika timu nne bora.

Timu zingine zinazopambana kumaliza katika nafasi nne bora ni pamoja na Chelsea na Tottenham ambazo zina alama 58 kila mmoja.