SOKA

Manchester United waomba City kufungwa mchuano mmoja ili wajihakikishie ubingwa

Manchester United huenda wakanyakua ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza wiki ijayo ikiwa wapinzani wao wa karibu Manchester City watapoteza mchuano wao dhidi ya Tottenham Hotsours mwishoni mwa juma.

Matangazo ya kibiashara

United walishindwa kujiongezea matumaini ya kujinyakulia taji hilo kabla ya ligi kukamilika baada ya kutoka sare ya mabao 2 kwa 2 na West Ham Jumatano usiku, huku Manchester City wakipata ushindi mwembamba wa bao 1 kwa 0 dhidi ya Wigan Athletic.

Hadi sasa, Manchester United inaongoza msururu wa ligi kwa alama 81 ikifuatwa na mabingwa watetezi Manchester City ambao wana alama 68 alama 13 nyuma ya United, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Chelsea ambayo ina alama 61 baada ya kuishinda Fulham mabao 3 kwa 0.

Ikiwa Manchester United itaishinda Aston Villa Jumatatu ijayo watakopowakaribisha Aston Villa katika uwanja wao wa Old Trafford  huenda wakatangazwa mapema kama mabingwa wa taji hilo.

Manchester City nao watatumai kuwa wataendelea kushinda mechi zote zilizosalia na kuomba Manchester United wanapoteza michuano yao yote ili kuona ikiwa wanaweza kutetea taji hilo.

Vlabu vya Chelsea, Tottenham Hotspurs, Asrsenal na Chelsea navyo vinawania kumaliza katika nafasi ya nne bora ili kushiriki kwenye mashindano ya kuwania taji la klabu bingwa barani ulaya UEFA.

Arsenal ni ya nne kwa alama 60, Spurs ni ya tano kwa alama 58 huku Everton ikiwa katika nafasi ya sita kwa alama 56.

Michuano ya mwisho ya ligi kuu nchini Uingereza itachezwa tarehe 19 mwezi ujao wa tano.