SOKA

Mabao ya Van Persie yaipaisha Manchester United

www.soccerbyives.net

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi Robin Van Persie ameiwezesha klabu ya soka ya Uingereza Manchester United kutwaa ubingwa wa 20 wa ligi kuu ya soka ya nchini Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Van Persie aliipatia United ushindi huo baada ya kupachika kimiani mabao matatu ndani ya dakika 31 za kipindi cha kwanza cha mechi iliyopigwa kwenye dimba la Old Traford dhidi ya ya Aston Villa.

United wamesalia na michezo mingine minne na tayari wamefikisha tofauti ya pointi 16 na waliokuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo Manchester City. huku wakiwa na michezo minne kibindoni.

Van Persie amefikisha idadi ya mabao 24 na anaongoza safu ya ufungaji akifuatiwa na Luis Suarez mwenye mabao 23 mpaka sasa.