HISPANIA

Cristiano Ronaldo tayari kuwakabili Borussia Dortmund kesho

REUTERS/Gustau Nacarino

Mshambuliaji nguli wa Klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo sasa atashuka dimbani wakati timu yake itakua ikikabiliana na timu ya Borussia Dortmund katika mchezo wao pili wa nusu fainali ya mabingwa wa Ulaya.

Matangazo ya kibiashara

Awali kulikua na wasiwasi kuwa huenda mchezaji huyo angekosa mechi hiyo ya kukata na shoka kutokana na maumivu ambayo yalisababisha kukosa mechi ya ligi kuu ya Hispania, La Liga walipoceza na Atletico Madrid na kupata ushindi wa 2-1.

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amesema kuwa Ronaldo atarejea uwanjani baada ya misuli iliyokua ikimsumbua kupona na anaanza mazoezi wenzake.

Ronaldo aliumia wiki iliyopita wa katika mchezo baina ya timu yake na Borussia Dortmund ya Ujerumani na kukubali kuzabwa bao 4-1 katika mchezo wa kwanza ambao ulifanyika ugenini.

Kocha Mourhino amesema kuwa Ronaldo yuko tayari kwa mchezo huo wa kesho na ameahidi kufanya maajabu huku akisema kuwa ana kikosi kamili cha kukabiliana na Borussia Dortmund.