HISPANIA

Jose Mourinho kung'oka Real Madrid baada ya vijana wake kuondolewa Klabu Bingwa Ulaya?

RFI

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho, amesema huenda akabwaga manyanga katika kibarua cha kuinoa klabu hiyo msimu ujao.

Matangazo ya kibiashara

Wasiwasi huo unakuja baada jana Jumanne, kushuhudia vijana wake wakiondolewa kwenye nusu fainali ya michuano ya kuwania kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya.

Real Madrid iliondolewa katika hatua hiyo licha ya kuilaza Borussia Dortmund ya Ujerumani, kwa magoli 2-0 na hivyo Dortmund ilifanikiwa kufuzu kwa fainali ya kombe hilo kwa jumla ya magoli 4-3.

Katika mechi ya awali Dortmund, iliibamiza Real Madrid kwa magoli 4-1 hatua ambayo imeisaidia timu hiyo kusonga mbele.

Kumekuwa ya ripoti kuwa kocha huyo kutoka Ureno alikua na mpango kuihama klabu ya Real Madrid na kurejea nchini Uingereza ambako anahisi anapendwa na mashabiki wengi pamoja na vyombo vya habari.