UINGEREZA

Gareth Bale awa mchezaji bora wa mwaka wa tuzo ya waandishi wa habari wa mpira wa miguu

Tottenham Hotspur ya Bale Gareth ametajwa kuwa Mchezaji bora wa mwaka Chama Waandishi wa habari z soka nchini Uingereza akichukua nafasi ya Robin van Persie aliyechukua nafasi hiyo mwaka jana.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Gareth Balemwenye umri wa miaka 23 alishinda tuzo nyingine ya mchezaji wa kulipwa iliyotolewa na chama cha wachezaji wa kulipwa wa kimataifa na tuzo ya mchezaji mdogo wa Mwaka alizoshinda wiki iliyopita.

Bale amefunga magoli 19 katika mechi 29 za Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu na hivyo kujizolea sifa kwa msimu huu akiwaacha nyuma wachezaji mahiri kama akina Robin van Persie, Scott Parker, Wayne Rooney, Steven Gerrard na Cristiano Ronaldo.

Robin van Persiewa wa Manchester United ambaye ni mshindi wa mwaka jana akiwa Arsenal, amekuwa wa pili, na Juan Mata wa Chelsea ametwaa nafasi ya tatu.

Bale, ambaye alichukua 53% ya kura, amesema na heshima kubwa kupokea tuzo ya Mwaka kutoka Chama cha Waandishi wa habari za soka.