KLABU BINGWA ULAYA

Kocha wa Bayern Munich atamba kutwaa ubingwa Klab Bingwa Ulaya

Reuters

Kocha wa Klabu ya Bayern Munich Jupp Heynckes amesema kuwa kipigo walichokipata katika mechi ya fainali ya klabu bingwa Ulaya msimu uliopita kutoka kwa Chelsea utachochea timu yake kupata ushindi katika mchezo wa fainali ya mwaka huu itakapokwana na Borussia Dortmund.

Matangazo ya kibiashara

Bayern Munich itakutana na Borussia Dortmund baada ya hiyo jana kuilamba kwa jumla ya bao 7-0 katika michezo yote miwili nyumbani na ugenini Barcelona ya Hispania.

Kocha huyo amesema kuwa kuna mengi ya kujifunza katika ushindi na kushindwa na ana matumaini kuwa vijana wake watatumia uzoefu wa kushindwa katika fainali za mwaka jana na Chelsea ili kutwaa ubingwa wa mwaka huu.

Timu yoyote kati ya timu hizo mbili itakayoshinda itakua ni mara ya kwanza kwa timu ya Ujerumani kutwaa ubingwa huo tangu mwaka 2001 pale Bayern Munich ilipotwaa Ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya.