ULAYA

Chelsea yatinga fainali ligi ya europa baada yan kuinyuka FC Basel

RFI

Klabu ya soka ya Chelsea imefanikiwa kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya ligi ya Uropa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao matatu dhidi ya moja la FC Basel katika hatua ya nusu fainali kwenye mechi yao iliyopigwa siku ya alhamisi katika dimba la Stamford Bridge.

Matangazo ya kibiashara

Mabao ya Fernando Torres, Victor Moses na David Luiz katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mchezo huo yalitosha kuwapandisha Chelsea na kuwafanya kuwa na jumla ya mabao matano dhidi ya mawili ya FC Basel.
 

Chelsea ambao wameshindwa kufanya vizuri katika hatua ya makundi kwenye michuano ya UEFA wanajidhatiti ili waweze kufanya vizuri kwenye fainali za msimu huu wakati watakapochuana na Benfica.
 

Akizungumzia mtanange huo kocha wa Basel Murat Yakin amesema licha ya kipigo walichokipata wachezaji wake wameonyesha uwezo wao katika soka kwa kukabiliana vizuri na Chelsea.
 

Kocha wa mpito wa Chelsea Rafael Benitez anamatumaini ya kukiongoza vyema kikosi hicho katika fainali zinazowakabili licha ya ukosoaji ambao amekuwa akikumbana nao toka kwa mashabiki.