UINGEREZA

Alex Ferguson awataka wachezaji wake kuwa huru katika mechi za ligi kuu ya Uingereza zilizosalia

REUTERS/Phil Noble

Meneja wa klabu ya soka ya Manchester United sir Alex ferguson amewataka wachezaji wake kuwa uhuru zaidi katika mechi za ligi kuu ya soka ya nchini Uingereza zilizosalia msimu huu kwani tayari wameshatwaa ubingwa wa 20 katika historia ya michuano hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Licha ya ubingwa wa mapema waliojinyakuliua, Ferguson amewasihi wachezaji wake kuwa makini na kulinda heshima waliyojiwekea msimu huu wakati watakapokutana na Chelsea katika dimba la Old Trafford jumapili hii.

United watacheza bila mshambuliaji wao Danny Welbeck ingawa kumekuwapo na taarifa kuwa kiungo Paul Scholes aliyekuwa akikabiliwa na majeraha ya goti toka mwezi January yupo tayari kushuka dimbani kwa sasa.

Manchester United sasa wanasubiri kombe lao la ligi kuu watakalokabidhiwa tarehe 13 ya mwezi huu ambayo itakuwa ni siku moja tu baada ya mchezo wao mwisho na Swansea kwenye dimba la nyumbani la Old Traford siku ya tarehe 12 mwezi huu.