UINGEREZA-UEFA

Kocha wa Chelsea Rafael Benitez anaamini timu yake itafuzu kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu ujao

Kocha wa Mpito wa Chelsea Rafael Benitez anaamini wamekaribia kupata tiketi ya kushiriki kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Manchester United. Benitez ameridhishwa na ushindi huo dhidi ya Manchester United ambao umeongeza matumaini katika klabu ya Chelsea kupata nafasi nne za juu ili waweze kushiriki kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya mwakani.

Kocha wa Mpito wa Cheslea Rafa Benitez anakiri timu yake inanafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya
Kocha wa Mpito wa Cheslea Rafa Benitez anakiri timu yake inanafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo wa Mpito amesema kwa sasa wanajiandaa kwa mchezo dhidi ya Tottenham huku akieleza iwapo watashinda mchezo huo watakuwa wameshajihakikishia kupata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa.

Benitez amesema wanamchezo mgumu sana mbele yao hivyo licha ya ushindi dhidi ya Manchester United lakini wanaangalia mchezo wao na Tottenham ambao nao wanawania nafasi hizo nne za juu pamoja na Arsenal.

Kocha huyo amesema wanajua pointi tatu dhidi ya Manchester United zilikuwa muhimu sana kwa upande wao lakini wanahitaji ushindi zaidi katika michezo ijayo ili wapate nafasi ya kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Chelsea inapigana kufa na kupona kuhakikisha inapata nafasi nne za juu kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza ili ipate nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya huku wakiwa na kumbukumbu ya kuondolewa kwenye hatua za mwanzoni mwaka huu.

Kikosi cha Benitez kitakuwa kinashuka dimbani kukabiliana na timu ya Andre Villas-Boas ambao nao wanasaka kwa udi na uvumba nafasi ya kushirikia Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya msimu ujao.

Chelsea walifanikiwa kupata ushindi wa goli moja kwa nunge mbele ya Manchester United katika mchezo uliopigwa dimbani Old Trafford kwa goli la kujifunga la Phil Jones baada ya kupigwa mpira na Juan Mata.