UHISPANIA-LA LIGA

Messi afunga mara mbili Barcelona ikikaribia kutwa Kombe la La Liga msimu huu dhidi ya Real Madrid

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akishangilia pamoja na wachezaji wenzake baada ya kufunga dhidi ya Real Betis
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi akishangilia pamoja na wachezaji wenzake baada ya kufunga dhidi ya Real Betis

Klabu ya Barcelona ya nchini Uhispania imeanza kukaribia kutwa taji la nchi hiyo baada ya kupata uhsindi wao dhidi ya Real Betis kipindi hiki michezo minne pekee imesalia kabla ya kumalizika kwa msimu huu.

Matangazo ya kibiashara

Barcelona imeanza kupata harufu ya kuibuka mabingwa msimu huu baada ya ushindi huo uliowaacha kuendelea kuongoza kwa tofauti kumi na moja mbele ya mahasimu wao wakubwa Real Madrid.

Lionel Messi ndiye alikuwa shujaa kwenye mchezo huo dhidi ya Real Betis baada ya kufanikiwa kufunga magoli mawili katia ya yale manne ambayo timu yake ilifanikiwa kuibuka kidede kwenye mchezo huo.

Messi alikuwa mwiba kwa mabeki wa Real Betis akitokea benchi na kufanikiwa kuisaidia Barcelona ambayo ilionekana bado inaendelea kuandamwa na jinamizi la kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya na Bayern Munich.

Barcelona inahitaji kupata ushindi katika mchezo wake ujao au itabidi waombe mahasimu wao Real Madrid wapoteze mchezo wao ujao ili wafanikiwe kutwaa ubingwa mapema zaidi kinyume na hapo watachelewa kuchukua taji hilo.

Messi baada ya kufunga magoli hayo mawili hayo jana amefikisha magoli 60 msimu huu kati ya hayo 46 amefunga kwenye Ligi Kuu maarufu kama La Liga akifutwa na Cristiano Ronaldo mwenye magoli 33.

Real Betis ndiyo walikuwa wa kwanza kufunga kwenye mchezo huo dhidi ya Barcelona kupitia Mshambulizji wake Dorlan Pabon kabla ya Alexis Sanchez hajasawazisha na kurejesha matumaini ya timu hiyo kupata ushindi.

Mshambuliaji Ruben Perez ndiye alifunga goli la pili la Real Betis kabla ya David Villa hajasawazisha tena na ndipo Messi alipoingia na kuisaidia Barcelona kuibuka na ushindi huo muhimu kwao.