UHISPANIA-LA LIGA

Kocha wa Barcelona Tito Vilanova anarejea New York kufanyiwa uchunguzi wa matibabu ya saratani ya koo aliyofanyiwa

Kocha Mkuu wa Barcelona Tito Vilanova akiwajibika Uwanjani na anatarajiwa kuendelea kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya koo inayomsumbua
Kocha Mkuu wa Barcelona Tito Vilanova akiwajibika Uwanjani na anatarajiwa kuendelea kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya koo inayomsumbua

Kocha Mkuu wa Mabingwa Watarajiwa Ligi Kuu nchini Uhispania maarufu kama La Liga Barcelona Tito Vilanova anatarajiwa kuelekea nchini Marekani juma hili kufanyiwa uchunguzi baada ya kupatiwa matibabu ya saratani ya koo inayomsumbua.

Matangazo ya kibiashara

Vilanova mwenye umri wa miaka 44 hakuwepo kwenye benchi siku ya jumapili wakati Kikosi chake kikipata ushindi dhidi ya Real Betis na kukaribia kutwaa taji la Uhispania msimu huu kama watapata pointi moja katika mchezo wao ujao.

Kocha wa Barcelona anarejea tena nchini Marekani katika Jiji la New York alipofanyiwa upasuaji mwezi Desemba na hivyo wataalam wanataka kufanya uchunguzi kubaini maendeleo ya upasuaji waliomfanyia.

Vilanova amewaambia wanahabari anaeleka New York kwa ajili ua uchunguzi zaidi na anatarajia kurejea tena nchini Uhispania siku ya alhamisi kuendelea na kazi yake iwapo atapewa ruhusa na Madakatari.

Barcelona wanahitaji pointi moja ili washinde taji mwishoni mwa juma hili na iwapo watafanikiwa kutwaa taji hilo ni wazi kabisa Vilanova atakosa sherehe hizo za kusherehekea ubingwa wa msimu huu.

Francesc “Tito” Vilanova ni miongoni mwa wachezaji waliovumbuliwa na Chuo cha michezo cha barcelona maarufu kwa jina la La Masia ambapo alicheza pamoja na Pep Guardiola aliyekuwa anainoa timu hiyo kabla ya kumkabidhi mikoba.

Vilanova aliondoka katika kikosi cha Barcelona na kujiunga na Timu ya Celta Vigo na kucheza kwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya kurejea tena katika kikosi B cha ambapo alianza kazi ya kufundisha.

Kocha huyo alishuhudia Kikosi cha Barcelona kikiondolowa kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya baada ya kufungwa kwa jumla ya magoli 7-0 mbele ya Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.