UINGEREZA-SOKA

Kocha wa Sunderland Di Canio awataka wachezaji wake kupigana kufa na kupona kwenye wao dhidi ya Southampton utakaopigwa Jumapili

Kocha Mkuu wa Sunderland Paolo Di Canio akizungumza na wanahabari baada ya mchezo wao na Stoke City
Kocha Mkuu wa Sunderland Paolo Di Canio akizungumza na wanahabari baada ya mchezo wao na Stoke City

Kocha Mkuu wa Sunderland Paolo Di Canio amesema wanajipanga kwa mchezo wa jumapili dhiid ya Southampton ambao wanauangalia kama mchezo wa fainali ili waweze kusalia kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza msimu ujao. Sunderland itashuka dimbani kukabiliana na Southampton ambayo nayo inapigana kufa na kupona kuepuska kushuka daraja ikiwa katika nafasi ya kumi na nne ikiwa ni pointi moja zaidi ya Paka hao Weusi.

Matangazo ya kibiashara

Di Canio ametoa kauli hiyo baada ya mchezo wao dhidi ya Stoke City ulioisha kwa sare ya magoli 1-1 na hivyo kuendelea kujiweka katika eneo la hatari ya huenda wakashuka daraja kama hawatapigana vilivyo kwenye michezo yao miwili iliyosalia.

Kocha huyo wa Sunderland anasema iwapo watashinda mchezo huo na kufikisha pointi arobaini na moja basi watakuwa salama na hawataweza kushuka daraja tena msimu huu na hivyo lazima wapambane kushinda mchezo huo muhimu kwao.

Sunderland imesalia na mchezo dhidi ya Southampton utakaopigwa siku ya jumapili kabla ya kumaliza mchezo wao wa mwisho kwenye siku ya mwisho wa kumalizika kwa Ligi ya msimu huu dhidi ya Tottenham.

Kocha wa Sunderland Di Canio amesema mchezo wa nyumbani dhidi ya Southampton ndiyo muhimu zaidi kuhakikisha mustakabali wao wa kusalia msimu ujao unatambulika kabla ya mchezo wa mwisho watakaocheza ugenini.

Sunderland inashika nafasi ya kumi na tano ikiwa na pointi thelathini na nane sawa kabisa Norwich na Newcastle United ambazo nazo zinapigana kuepuka kushuka daraja huku Wigan Athletic ina pointi thelathini na tano lakini haijacheza mchezo mmoja.

Wigan inatarajiwa kushuka dimbani hii leo kucheza na Swansea ambapo kama itashinda nayo itakuwa imeongeza shinikizo kwa timu ambazo zinaendelea kupambana kuepuka kushuka daraja msimu huu.

Di Canio amepongeza timu yake namna ilivyoweza kupigana kufa na kupona katika kuhakikisha inapatapointi kwenye mchezo wao dhidi ya Stoke City licha ya kucheza wakiwa na wachezaji kumi baada ya Craig Gardner kulimwa kadi nyekundu.

Tangu Di Canio ajiunge na Sunderland amefanikiwa kushinda michezo miwili, amefungwa michezo miwili na kuambulia sare moja aliyopata katika mchezo wa jana akiendelea kupigana kuiokoa timu hiyo isishuke daraja.