UINGEREZA

Wigan yaizamisha Man City katika fainali za kombe la FA

Reuters

Klabu ya soka ya Manchester City imepata kipigo cha bao1-0 toka kwa Wigan Athletic katika mechi ya fainali ya kombe la FA iliyopigwa jumamosi hii kwenye dimba la Wembley.

Matangazo ya kibiashara

Bao la ushindi la Wigan lilipachikwa kimiani na Ben Watson katika dakika za lala salama baada ya kuunganisha vizuri kona iliyochongwa na Shanu Maloney hatua iliyoamsha furaha ya mashabiki wao na kusababisha wasahau kipigo walichokipata katika michuano ya ligi kuu.

Wigan wa wametinga fainali za FA katika msimu huu kwa mara ya kwanza na wametwaa ushindi wa taji hilo kwa mara ya kwanza katika miaka 81 ya historia yao ya michuano ya soka.

Man City ambao ni mabingwa wa FA katika msimu uliopita wanamaliza vibaya msimu huu baada ya kugaragazwa katika michuano ya ligi kuu na pia kutolewa katika hatua ya makundi kwenye michuano ya klabu bingwa wakati mahasimu wao Manchester United wakineemeka na taji la 20 la ubingwa ligi kuu ya Uingereza.