SOKA

Drogba awafungukia mashabiki wa Fenerbach baada ya kumkashifu kwa kumwonyesha ndizi

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini cote d'ivoire Didier Drogba ambae anakipiga katika klabu ya Galatasaray kule nchini Uturuki amejibu kashfa za ubaguzi wa rangi zilizo tolewa na mashabiki wa klabu ya Fenerbach juzi Jumapili wakati wa mechi baina ya Galatasaray na Fenerbach ambapo timu hizo zilifungana mabao mawili kwa moja.  

Didier Drogba mshambuliaji wa timu ya Galatasaray ya Uturuki
Didier Drogba mshambuliaji wa timu ya Galatasaray ya Uturuki gurdian.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Drogba ameandika katika mtandao wa kijamii wa Instagram akiwakumusha mashabiki jinsi walivyo mshangilia na kumpongeza wakati alipotwaa ubingwa wa ulaya, na alipokuwa bingwa wa Uturuki katika klabu ya Galatasaray.

Drogba na mwenzake Emmanuel Eboue walizomewa na mashabiki wa Fenerbach na kuonyeshwa ndizi, ishara ya nyani wakati wa mechi ya kabla ya mwisho wa ligi ambapo shabiki mmoja wa Fenerbach aliuawa kwa kudungwa kisu na shabiki wa Galatasaray, ambae hata hivyo polisi imemtia nguvuni.