SOKA

Lionel Messi kutoshiriki michuano katika klabu yake kutokana na majeraha

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi telegraph.co.uk

Mshambuliaji bingwa namba tatu wa mpira wa dhahabu, Lionel Messi wa klabu ya Barcelona ya kule Uhispania, huenda huu ukawa ndio mwisho wa msimu kwa mchezaji huyo, baada ya mara kadhaa kuwekwa kando katika timu hiyo kutokana na majeraha.

Matangazo ya kibiashara

Jumapili hii Messi alilazimika kutolewa nje ya uwanja baada ya kujeruhiwa wakati timu yake ilipokuwa ikipepetana na Atletico Madrid.

Messi anasumbuliwa na mguu wa kushoto na amepewa mapumziko yanayoweza kwenda hadi majuma mawili au matatu wakati Barcelona inatarajiwa kucheza mechi yake ya mwisho ya ligi kuu nchini Uhispania Juni Mosi mwaka huu.