Michezo

Andy Murray kutoshiriki mashindano ya French Open

Bingwa namba tatu wa tennis duniani Andy Murray
Bingwa namba tatu wa tennis duniani Andy Murray in.reuters.com

Bingwa namba mbili duniani kwenye mchezo wa tennis Andy Murray amekiri kwamba anweza akakosa mashindano ya French Open kutokana na jeraha la muda mrefu ambalo lilimlazimisha kujiondoa kwenye mashindano ya Rome Masters. 

Matangazo ya kibiashara

Murray ambaye ameadhimisha miaka 26 ya kuzaliwa kwake jana Jumatano, amesema kuwa maumivu chini ya mgogo upande wa kushoto ambayo yamemsumbua tangu mwaka 2011 yameongezeka hivi karibuni na kumfanya ashindwe kuendelea na mashindano ya Roma.

Kwa upande wa wanawake Wakati huo huo mcheza tennis kwa upande wa wanawake bingwa namba moja Li Na amefuzu katika hatua ya tatu ya mashindano ya rome Open jana Jumatano baada ya kumshinda mpinzani wake Zheng Jie ambaye anamtaja kama pacha wake kwa seti 6-3, 6-1