ULAYA

David Beckham kustaafu soka la kulipwa la kimataifa

David Bechkam
David Bechkam thetimes.co.uk

Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza David Beckam aliyekuwa anakipiga na Paris Saint German, ametangaza kuwa atastaafu soka la kulipwa la kimataifa. 

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 amesema hataongeza mkataba na klabu ya Ufaransa iliyotwaa ubingwa msimu huu ya PSG ambayo ilikuwa tayari kumuongezea mkataba mwingine.

Akizungumza na Skynews David Beckam ameishukuru klabu hiyo kwa kumpa fursa ya kuendelea kukipiga katika klabu hiyo, lakini amesema ni wakati muafaka wa kustaafu soka la kimataifa akiwa katika hali nzuri kiafya.

Beckham anastafu soka la kimataifa baada ya Klabu yake ya PSG kutwaa ubingwa wa ligi kuu nchini Ufaransa baada ya kuitandika Lyon bao moja kwa nunge.

Mchezaji huyo ameandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Uingereza kutwaa ubingwa katika nchi nne tofauti.

Beckham alitwaa ubingwa akiwa na klabu ya mashetani wekundu Man United mwaka 1992 akiwa na umri wa miaka 17, mwaka 2003 na 2007 alitwaa ubingwa akiwa katika klabu ya Real Madrid na baadae alielekea nchini Marekani katika Klabu ya Los Angeles Galaxy ambapo klabu hiyo ilitwaa ubingwa na hatimaye ni ubingwa wa hivi majuzi na Klabu ya Paris Saint German.

Beckham atacheza mechi yake ya mwisho ya kimataifa tarehe 26 Mei wakati klabu yake ya PSG itakapo menyana na Lorient