ULAYA

Rafael Benitez asema anajivunia kuinoa Chelsea

Kocha wa Chelsea, Rafael Benitez akifurahia ushindi pamoja na vijana wake
Kocha wa Chelsea, Rafael Benitez akifurahia ushindi pamoja na vijana wake gurdian.co.uk

Kocha wa klabu ya Chelsea Rafael Benitez amesema kuwa anajivunia kuwa katika klabu hiyo baada ya kuiongoza hadi kutwaa kombe la Europa League baada ya kuichabanga klabu ya Benfica kwa magoli 2-1 katika fainali za kombe hilo kwenye dimba la Amsterdam Arena. 

Matangazo ya kibiashara

Benitez amesema kuwani jambo la kujivunia kama kocha kuingia katika kipindi cha pili wakiongoza kwa goli lililofungwa na Fernando Torres kabla ya kurejeshwa nyuma kwa mkwaju wa penati uliopigwana Oscar Cardozo na hatimaye Branislav Ivanovic kuifungia Chelsea bao la ushindi katika muda wa ziada.

Chelsea ililazimika kuondoa hofu haswa katika kipindi cha kwanza wakati timu ya Benfica ilipoonekana kutamba ingawa haikuweza kupata nafasi za kumiliki mpira na kufunga magoli.

Kocha huyo wa zamani wa klabu ya Liverpool ameendelea kutokuwa maarufu miongoni mwa mashabiki wa Chelsea tangu aliporithi mikoba ya Roberto Di Matteo mnamo mwezi November mwaka jana.