ITALIA

Bradley Wiggins ashindwa kuendela na mashindano ya Giro d'Italia kutokana na maumivu ya kifua

Mshindi wa tour de France mwaka 2012 Bradley Wiggins
Mshindi wa tour de France mwaka 2012 Bradley Wiggins dailymail.co.uk

Mshindi wa mwaka uliopita wa mashindano ya mbio za baskeli yajulikanayo kama Tour de France Bradley Wiggins amejiondoa katika mshindano ya Giro d'Italia kutokana na matatizo ya kiafya, timu yake imearifu leo Ijumaa. 

Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya timu hiyo imeeleza kuwa baada ya kukithiri kwa maambukizi kwenye kifua, uamuzi ulichukuliwa na kutomruhusu Wiggins kuanza mzunguko wa 13 wa mbio hizo leo Ijumaa kutoka Busseto hadi Cherasco.

Wiggins amesumbuka katika mbio baada ya maumivu ya kichwa kuhamia kifuani ambapo aliondoka katika kasi yake zaidi ya mara tatu wakati wa mzunguko wa 12 wa mbio hizo jana Alhamisi.

Mkuu wa timu yake Dave Brailsford amesema kuwa wamekuwa wamwangalia Wiggins tangu usiku hadi leo asubuhi na wameamua kumwondoa katika mashindano hayo bada ya kupata ushauri wa daktari wa timu.