Tanzania

Watani wa jadi Simba na Yanga kuvaana kesho uwanja wa Taifa

Mtanange wa ligi kuu ya Vodacom kati ya watani wa jadi Simba na Yanga za nchini Tanzania unatarajiwa kutimua vumbi kesho Jumamosi kwenye uwanja wa taifa hilo jijini Dar es Salaam. 

Simba na Yanga
Simba na Yanga globalpublishers.com
Matangazo ya kibiashara

Tiketi za mpambano huo tayari zimeanza kuuzwa kwenye vituo mbalimbali tangu majira ya saa tatu asubuhi hadi saa majira ya jioni ili kuwawezesha mashabiki kushuhudia mtanange huo.

Mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania wameripotiwa kufurika vituoni kuwahi tiketi za mpambano huo wa kufunga pazia la ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa.

Yanga wanashuka uwanjani wakiwa tayari wamejipatia ushindi huku Simba ikikamilisha ratiba baada ya kukosa alama muhimu za kuiwezesha kupata ushindi katika mechi zilizopita.