ULAYA

Atletico yailaza Real Madrid 2-1

Timu ya Atletico Madrid imeshinda kombe la kumi la Uhispania jana Ijumaa baada ya kuichapa vibaya timu pinzani ya Real Madrid kwa magoli 2-1 katika muda wa ziada wakati wa mechi ambayo ilishuhudia kocha Jose Mourinho na Christiano Ronaldo wakiondolewa. 

Mtanange kati ya Real Madrid na Atletico Madrid
Mtanange kati ya Real Madrid na Atletico Madrid dailymail.co.uk
Matangazo ya kibiashara

Timu ya Real imekuwa ngumu kufungwa kwa mara 25 katika kipindi kilichopita wakati timu hizo zinapokutana kwa kipindi cha miaka 14 ambapo vijana wa Mourinho walianza vema baada ya Ronaldo kupata nafasi kupitia kona iliyotengenezwa na Luka Modric.
Hata hivyo Dioego Costa alisawazisha bao hilo dakika kumi kabla ya nusu ya kwanza ya mchezo huo na mshambuliaji Los Rojiblancos kujazia bahati yao ya ushindi baada ya wachezaji wa Real Metus Ozil, Karim Benzema na Ronaldo kukosa penati baada ya kugonga post.

Mourinho ambaye anatarajiwa kurejea kuinoa Klabu ya Chelsea katika msimu ujao , aliondolewa kwenye benchi la ufundi dakika 13 baada ya kumalizika kwa muda rasmi wa mchezo kabla ya Miranda kuiongoza Atletico kutwaa ushindi dakika nane za muda wa ziada.

Aidha Ronaldo alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupokea kwa ukali hatua ya ucheleweshwaji wa mpira iliyofanywa na mchezaji wa Atletico zikiwa zimesalia dakika sita.