Ufaransa

Marion Bartoli na Tamira Paskez waondolewa mashindano ya kimataifa ya tenisi ya Strasbourg

Mchezaji namba moja Marion Bartoli na namba mbili Tamira Paskez katika mchezo wa tenisi  wameondolewa katika mzunguko wa kwanza wa mashindano ya Kimataifa ya Strasbourg nchini Ufaransa leo Jumanne. 

Marion Bartoli mchezaji aliyeondolewa katika mzunguko wa kwanza wa Strasbourg
Marion Bartoli mchezaji aliyeondolewa katika mzunguko wa kwanza wa Strasbourg hindustantimes.com
Matangazo ya kibiashara

Bartoli, aliyefuzu fainali za mashindano ya Wimbledon finalist, alipoteza mchezo wake baada ya kufungwa na Camila Giorgi kwa seti 6-3, 6-2, wakati Paszek akifungwa na Mfaransa Virgine Razzano kwa seti 6-1, 6-4.

Pia, mchezaji namba sita Christina McHale alipoteza mchezo kwa kufungwa na Lauren Davis kwa seti 7-5, 6-3, wakati Eugenie Bouchard, Johanna Larsson, Lucie Hradecka, Magda Linette na Shelby Rogers wakisonga mbele.

Mvua kubwa imezuia michezo yote ya jana jumatatu na kulazimisha mechi saba za mzunguko wa kwanza kuchezwa leo Jumanne