michezo

Majeraha ya mgongo yamuweka Andy Murry nje ya michuano ya French Open

Mcheza Tennis Bingwa nambari mbili duniani Andy Murray,majeraha yamuweka nje ya French Open safari hii
Mcheza Tennis Bingwa nambari mbili duniani Andy Murray,majeraha yamuweka nje ya French Open safari hii

Andy Murray amejiondoa katika mchuano wa French Open kutokana na majeraha mgongoni kumlazimu kufanya hivyo akiwa Italia Juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo bingwa nambari mbili katika Tennis ulimwenguni amesitisha mechi yake ya kwanza huko Roma.

Hata hivyo Murray amesema anamatarajio ya kupata ahueni na kushiriki kuanza kwa msimu mpya wa mchuano utakao fanyikia Queen's Club mnamo tarehe 10 mwezi June.

''Kwa hakika ni maamuzi magumu ,na napenda kuchezea Paris lakini kwa mujibu wa ushauri wa kitabibu afya yangu hainiruhusu kushindana.''alisema Murry na kuomba radhi kwa waandaaji huku akiwashukuru mashabiki wote kwa kumuunga mkono.

Hii ni kwa mara ya kwanza kwa bingwa huyo wa tennis kukosa kushiriki michuano ya Grand Slam tangu ile ya Wimbledon mwaka 2007.

Michuano ya French Open, tuzo ya pili ya Grand Slam kwa mwaka inaanza kurindima jumapili ijayo huko Roland Garros.