Michezo

Adriano aingia mkataba mpya wa miaka minne Barcelona

Mchezaji Adriano Correia amekubali kuongeza mkataba wa miaka minne hadi kufikia mwaka 2017 mabingwa wa La Liga Barcelona walibainisha katika taarifa yao.

Adriano Correia ambaye ameongeza muda wa kuichezea  Barcelona
Adriano Correia ambaye ameongeza muda wa kuichezea Barcelona REUTERS/Gustau Nacarino
Matangazo ya kibiashara

Raia huyo wa Brazili ambaye ameingia mkataba kutoka Sevilla mwaka 2010, amekubali mkataba kwa kitita cha yuro milioni 90.

Duru zimebainisha kuwa Adriano amejipatia umaarufu kupitia umahiri wake mara zote alizochezea msimu wa Barca.

Adriano amesakata kabumbu vema mara zote akiwa mchezaji wa kati na eneo la nyuma,bila kusahau kulia na kushoto amekuwa makini hata akiwa kiungo mshambuliaji.

Adriano mwenye umri wa miaka 28 ambaye amehamia nafasi ya ulinzi wa kati kwa lengo la kusaidia kuponya majeraha msimu huu ameshafanikiwa kupata magoli 10 katika mechi 105 alizochezea Barcelona.