Michezo

Rio Ferdinand aongeza mkataba wake mwaka mmoja zaidi Manchester United.

Beki wa muda mrefu wa klabu ya soka ya Manchester United Rio Ferdinand amesaini mkataba wa mwaka mmoja zaidi katika klabu hiyo,Mktaba ambao umethibitishwa na kocha mpya wa klabu David Moyes na kumaliza mazungumzo ambayo yamekuwa yakiendelea katika klabu hiyo ikiwa ataendelea kuichezea klabu hiyo msimu ujao.

Mchezaji Rio Ferdinand ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja Manchester United
Mchezaji Rio Ferdinand ambaye ameongeza mkataba wa mwaka mmoja Manchester United footballfancast.com
Matangazo ya kibiashara

Ferdinand mwenye umri wa miaka 34 ameichezea Manchester United mara 34 msimu uliopita ikiwemo mara 28 katika michuano ya ligi kuu nchini himo.

Beki huyo ameisaidia timu yake kunyakua mataji 6 ya ligi kuu ya soka nchini humo ikiwemo taji la mwaka huu pamoja na kombe la dunia bao la vilabu vya soka mwaka 2008 na ile ya klabu bingwa barani Ulaya mwaka 2007.

Mchezaji huyo alijiunga na United mwaka 2002 kutokea klabu ya West Hama baada ya kusajiliwa kwa Puani Milioni 30 akiwa mojawapo ya mchezaji aliyesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha duniani kipindi hicho.

Licha ya kuichezea Manchester United mara 432 Ferndinad ameichezea Uingereza mara 81.